Ghorofa ya kwanza kwa juu
söndag 5 april 2015
Huu ni mradi wa ujenzi wa madrasa ya wasichana ambao ni mayatima ulioanzishwa na juhudi za watu wawili binafsi. Tulianzisha fikra za kuwalea wasichana mayatima wa Kiislamu tangu 2013 katika nyumba ya kupanga. Na ilipofika 2014 tukajiwa na fikra za kujenga madrasa yetu ambapo mayatima hao watakuwa wanaeshi na kusoma masuala mbali mbali yanayohusiana na dini yao. Tunamshukuru Allaah kuanzia wiki hii tarehe 16.03.2015 mradi huo wa kujenga madrasa ulianza na mpaka sasa tunazidi kupiga tambo mbele.
Mradi wetu huu hautegemei msaada kutoka kwenye chama, taasisi, jumuiya wala kundi lolote na wala hautaki msaada na mchango huo na khaswa ikiwa ni kutoka kwa watu wenye fikra potofu na walopinda. Ni juhudi zinazoendeshwa na watu binafsi. Hata hivyo yule atayependa kusaidia na kutoa mchango wake ili kuziendeleza juhudi hizi anakaribishwa kwa kile ambacho Allaah atakuwa amemuwezesha. Ijulikane kuwa kila yule ambaye atatoa pesa yake 1 tu basi bila ya shaka yoyote kabisa twamyakinisha kuwa itaenda katika kazi yake stahiki. wa billaahi at-Tawfiyq
Tanbihi! Madrasa hayo yamejengwa juu ya msingi wa kufuata Qur-aan, Sunnah kwa ufahamu wa Salaf-us-Swaalih (wema waliotangulia).
Tanbihi! Madrasa hayo yamejengwa juu ya msingi wa kufuata Qur-aan, Sunnah kwa ufahamu wa Salaf-us-Swaalih (wema waliotangulia).
Prenumerera på:
Inlägg (Atom)